Udhibiti wa viduha
- 8 years ago
- 17832 Views
-
ReportNeed to report the video?Sign in to report inappropriate content..
Viduha ni gugu hatari lililo/sambaa kwa wingi na linaloshambulia mpunga wa milimani katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara .Video hii inaelezea kanuni bora za kilimo zinazoweza kutumiwa kusaidia wakulima wa mpunga ili kupunguza tatizo la viduha katika mashamba yao. Video hii ya dakika 21 inaonesha kanuni nne tofauti zinazoweza kusaidia kupunguza tatizo la viduha mashambani:1. Kupanda mazao kwa mzunguko au kwa mseto na mimea jamii ya kunde2. Kupanda mbegu moja kwa moja kwenye shamba lenye mabaki ya mazao ya msimu uliopita bila kulima au kutifua udongo3. Kurutubisha udongo kwa kutumia mbolea za viwandani na zile za asili4. Kutumia mbegu za mpunga zenye ukinzani dhidi ya Kiduha.Kanuni tatu za kwanza zina manufaa makubwa katika uhifadhi na kuongeza rutuba ya udongo. Wakulima wanaelezea kwa maneno yao wenyewe uzoefu walioupata kwa kufuata kanuni hizi na kueleza sababu za kuzifuata na kwa namna gani inatakiwa kufanyika.Video hii inapatikana katika lugha tano ambazo ni Kifaransa, Kimalagasi , Kiingereza, Kiswahili na Kireno .Washirika : AfricaRice , CIRAD , FOFIFA , GSDM ; Wafadhili : AfDB , kupitia mradi Sard - SC .
Login or Signup to post comments